MSHAMBULIAJI wa West Ham United, Andy Carroll ameshindwa rufani yake ya kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo dhidi ya Swansea Jumamosi iliyopita baada ya Chama cha Soka cha Uingereza, FA kuitupilia mbali. Carroll mwenye umri wa miaka 25 alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kugongana na beki wa Swansea Chico Flores katika mchezo huo ambao West Ham waliibuka kidedea kwa kushinda mabao 2-0. Mshambuliaji huyo sasa atakosa mechi tatu za Ligi Kuu ambazo timu yake itacheza na Aston Villa, Norwich na Southampton. Kwa mujibu wa taarifa kutoka FA, West Ham wameshindwa kuwasilisha ushahidi kuwa mwamuzi Howard Webb aliyechezesha mchezo huo alifanya makosa kumtoa Carroll baada ya mkono wa nyota huyo kumpiga usoni Flores.
No comments:
Post a Comment