KLABU ya Shakhtar Donetski imethibitisha kuwa mshambuliaji wao Maicon Pereira de Oliveira amefariki dunia kwa ajali ya gari. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ukraine mwaka 2012 na alikuwa akicheza kwa mkopo katika timu ya Illichivets Mariupol. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo ilithibitisha taarifa hizo kuwa nyota huyo alifariki leo kwa ajali ya gari jijini Donetsk. Maicon alianza kucheza soka katika timu ya nyumbani kwao ya Fluminense kabla ya kuhamia Ukraine na kujiunga na timu ya Volyn Lutsk mwaka 2009 na kufunga mabao 30.
No comments:
Post a Comment