Tuesday, March 4, 2014

CARDIFF CITY MATATANI BAADA YA TAJIRI WAKE KUTOA OFA YA JANGUSHO.

LIGI Kuu nchini Uingereza inatarajia kuichunguza klabu ya Cardiff City baada ya mmiliki wake Vincent Tan kuahidi kutoa bakshishi ya paundi milioni 3.7 kwa wachezaji wake kabla ya mchezo waliofungwa na Tottenham Hotspurs Jumapili. Kwa mujibu wa sheria za ligi hiyo kila timu inapaswa kuwasilisha taratibu za kutoa bakshishi zao kabla ya kuanza kwa msimu hivyo Tan tayari amevinja sheria hiyo kwa kutoa bakshishi hiyo ili kuzuia timu yake isishuke daraja. Kwa mujibu wa mtandao wa Sportsmail tajiri huyo hakutoa bakshishi yoyote kwa kikosi cha Cardiff ili kuzuia isishuke daraja kabla ya msimu kuanza kwasababu hakuamini kama wanaweza kuwepo katika nafasi hiyo hivi sasa. Badala yake Tan alifanya ziara ya kuitembelea timu hiyo katika hoteli waliyofikia ya Hilton Jumamosi usiku na kutoa ofa hiyo kwa wachezaji ingawa hata hivyo haikusaidia sana kwani waliambulia kipigo.

No comments:

Post a Comment