Thursday, March 13, 2014

DJOKOVIC, FEDERER WATINGA ROBO FAINALI INDIAN WELLS.

WACHEZAJI nyota wa tenisi, Novak Djokovic na Roger Federer wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya wazi ya BNP Paribas huko Indian Wells. Djokovic raia wa Serbia anayeshika nafasi ya pili katika orodha za ubora alifanikiwa kutinga hatua hiyo kwa kumfunga Marin Cilic wa Croatia kwa 1-6 6-2 6-3 na sasa atachuana na Mfaransa Julien Benneteau. Bingwa mara 17 wa michuano ya Grand Slam Roger Federer naye alitinga hatua hiyo kwa kumgaragaza Tommy Haas ambapo ushindi huo utampeleka kupambana na Kevin Anderson wa Afrika Kusini aliyemtoa bingwa wa michuano ya wazi ya Australia Stanislas Wawrinka. Kwa upande wa wanawake Agnieszka Radwanska alifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa kumgaragaza Jelena Jankovic na sasa atakwaana na Simona Halep katika kutafuta nafasi ya kucheza fainali ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment