Saturday, March 22, 2014

GABRIEL HEINZE ATUNDIKA DARUGA.

MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Argentina, Gabriel Heinze ametangaza kutundika rasmi daruga zake kufuatia kusumbuliwa na mejruhi ya muda mrefu. Beki huyo aliyekuwa akicheza katika klabu ya Newell Odl Boys amekuwa akipambana na majeruhi katika vipindi tofauti kwa miaka kadhaa mpaka kufikia uamuzi huo akiwa na umri wa miaka 35 sasa. Katika taarifa yake ilichapishwa katika mtandao wa klabu hiyo Heinze amesema kwa masikitiko kuwa kama ilivyo kwa kila kitu katika maisha hata ndoto pia zina mwisho wake. Heinze amesema pamoja na kwamba anapenda kuendelea kuitumikia klabu hiyo lakini anadhani mwili wake umekataa kutokana na majeruhi ambayo ymekuwa hayamwishi. Nyota huyo aliushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa kipindi chote na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kadri atakavyohitajika. Heinze alianza soka lake kwa katika klabu hiyo kabla ya kutimkia Villadolid ya Hispania huku pia akicheza katika vilabu vya Paris Saint-Germain, Manchester United, Real Madrid, Olympique Marseile na Roma.

No comments:

Post a Comment