ALIYEKUWA nahodha wa timu ya taifa ya Brazil iliyonyakuwa taji la Kombe la Dunia mwaka 1958, Bellini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83. Beki huyo alikiongoza kikosi cha Brazil akiwemo Pele aliyekuwa na umri wa miaka 17 kuwagaragaza wenyeji Sweden kwa mabao 5-2 katika mchezo wa fainali na kuifanya nchi hiyo kunyakuwa taji hilo kwa mara ya kwanza. Nguli anapewa heshima kubwa nchini Brazil kwa kuwa nahodha wa kwanza kunyanyua juu Kombe la Dunia. Nguli amefariki kwa kinachohofiwa kuwa shinikizo la damu na maradhi mengine yanayowakuta watu wenye umri mkubwa. Rais wa Shirikisho la Soka nchini humo, Jose Maria Marin alituma salamu zake za rambirambi kwa familia ya nguli huyo na kumuelezea kama mtu muhimu na kiongozi imara kwa timu ya Brazil.
No comments:
Post a Comment