Thursday, March 13, 2014

PIRLO KUSAINI MKATABA MPYA JUVENTUS.

NYOTA wa klabu ya Juventus, Andrea Pirlo amesisitiza kuwa atasaini mkataba mpya na klabu hiyo katika siku za karibuni. Mkataba wa sasa wa kiungo huyo mkongwe unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na huku akiwa bado hajasaini mwingine hivyo kuzusha hofu. Hata hivyo Pirlo alibainisha kuwa kulikuwa na baadhi ya mambo katika mkataba mpya yaliyokuwa hayajawekwa sawa lakini amewahakikishia mashabiki wake kuwa bado ataiwakilisha Juventus msimu ujao. Pirlo amesema hana shaka kila kitu kitakaa sawa na kusaini mkataba mpya hivi karibuni huku pia akiondoa tetesi kuwa ana mahasiano yasiyo mazuri na kocha wake Antonio Conte.

No comments:

Post a Comment