BEKI wa klabu ya Barcelona, Dani Alves amedhihaki jinsi timu hiyo isivyopewa nafasi kwasasa na kudai kuwa wakishinda mechi mwamuzi lazima alaumiwe na wakifungwa watu wanadai ufalme wao umekwisha. Mwezi uliopita Barcelona waliteleza na watu kudhani kuwa mbio zao za kutetea ubingwa wa La Liga zilizkuwa zimekwisha lakini walifanikiwa kubadilika na kurejea katika mbio hizo kwa ushindi dhidi ya Real Madrid na Espanyol. Hata hivyo mechi zote mbili walizoshinda zimekuwa zikilalamikiwa kutokana na maamuzi yaliyotolewa na waamuzi baada ya mechi na Alves anafikiri kuwa hakuna uwezekano tena wa Barcelona kushinda bila kulalamikiwa. Alves amesema tuhuma kwa waamuzi zimekuwa zikiwapa ari kwasababu ni kawaida kwa ushindi wao kuelezewa hivyo ndio maana wamezoea hivi sasa. Barcelona leo itaikaribisha Atletico Madrid katika mchezo wa mkondo wa kwanza war obo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaofanyika katika Uwanja wa Camp Nou.
No comments:
Post a Comment