KLABU ya Arsenal imefanya mawasiliano na Louis van Gaal kutokana na kutokuwa na uhakika na mstakabaliwa kocha Arsene Wenger. Arsenal bado wana matumaini kuwa Wenger atasaini mkataba mpya wa miaka miwili waliokubaliana Octoba mwaka jana lakini inajulikana anaweza kujiuzulu kama akishindwa kufikia malengo aliyojiwekea baada ya kumalizika kwa msimu. Imebainika kuwa Mfaransa huyo aliwaambia marafiki zake kuwa anafikiria kuacha kuinoa Arsenal kama awatashinda Kombe la FA na kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu. Kutokana na hali hiyo kumekuwa na mipango ya muda mfupi inayofanywa na Arsenal, mojawapo ni kujaribu kufanya mazungumzo na Van Gaal ambaye mkataba wake na timu ya taifa ya Uholanzi unamalizika baada ya Kombe la Dunia. Mbali na kuwindwa na Arsenal, Van Gaal pia anawindwa na Manchester United na Tottenham Hotspurs ambao nao wanataka achukue nafasi ya Tim Sherwood mwishoni mwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment