MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Costa kuna hati hati ya kukosa mechi ya mkondo wa kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Barcelona baada ya kuwahi kuondoka mazoezini jana. Kocha wa Atletico Diego Simeone amedai kuwa itakuwa ni jambo gumu kwa Costa kucheza katika mchezo huo wa leo baada ya kufanya mazoezi kwa dakika 10 pekee na kuondoka kutokana na maumivu. Costa amekuwa sehemu muhimu katika kikosi cha Simeone akiwa amefunga mabao 32 katika mashindano yote msimu huu, yakiwemo mabao sita katika mechi tano zilizopita. Simeone amesema madaktari watamfanyia uchunguzi kama atakuwa fiti lakini hadhani kama atamjumuisha katika kikosi chake.
No comments:
Post a Comment