MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Hispania Diego Costa amefaulu vipimo vya afya katika klabu ya Chelsea kuelekea uhamisho wake utakaogharimu paundi milioni 32 kutoka Atletico Madrid. Chelsea imefanikiwa kufikia kifungu kilichowekwa katika mkataba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 na Atletico na sasa anatarajiwa kujadili masuala yake binafsi. Costa amefunga mabao 36 katika mechi 52 alizoichezea Atletico msimu huu na kuisadia kunyakuwa taji lao la kwanza la La Liga toka mwaka 1996 na pia kufikia hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Nyota huyo ambaye ni mzaliwa wa Brazil yuko katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment