Monday, June 2, 2014

QATAR KUKUTANA NA MPELELEZI WA FIFA KUHUSIANA NA KASHFA YA UFISADI.

WAANDAAJI wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar wanatarajia kukutana na mpelelezi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Michael Garcia leo kufuatia kuongezeka kwa wito wa kuitaka nchi hiyo ivuliwe haki ya kuandaa michuano hiyo. Gazeti la Sunday Times nchini Uingereza lilitoa taarifa kuwa kulitolewa mamilioni ya paundi kwa maofisa ili waiunge mkono timu hiyo katika kinyang’anyiro cha kutafuta nafasi ya kuandaa michuano hiyo. Makamu wa rais wa FIFA, Jim Boyce amesema ataunga mkono suala la upigaji kura tena kama tuhuma za ufisadi zitagunduliwa. Kamati iliyokuwa ikiongoza zoezi la kuhakikisha nchi hiyo inapata nafasi ya kuandaa michuano hiyo ilitoa taarifa jana ya kukaa tuhuma hizo zilizotolewa. Qatar ilizishinda nchi za Korea Kusini, Japan, Australia na Marekani na kushinda haki ya kuandaa michuano hiyo ya mwaka 2022.

No comments:

Post a Comment