KLABU ya Bayern Munich imemsajili beki wa kati Juan Bernat kutoka klabu ya Valencia kwa mkataba wa miaka mitano. Bayern hawakuweka wazi ada waliyomnunulia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye pia anaweza kucheza kama winga lakini vyombo vya habari nchini Ujerumani vimeripoti kuwa amenunuliwa kwa euro milioni 10. Mkurugenzi wa michezo wa Bayern, Matthias Sammer amesema Bernat ni mchezaji mdogo lakini mwenye kipaji cha hali ya juu na wamekuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu sasa. Bernat anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Bayern katika kipindi hiki cha usajili wamajira ya kiangazi akitanguliwa na Robert Lewandowski aliyetokea Borussia Dortmund na kiungo Sebastian Rode aliyetokea Eintracht Frankfurt. Winga huyo amecheza mechi 51 za La Liga akiwa na Valencia na pia alikuwemo katika kikosi cha cha timu ya taifa ya Hispania kwa vijana chini ya umri wa miaka 19 ambacho kilinyakuwa michuano ya Ulaya kwa vijana wa umri huo mwaka 2012 huko Estonia.
No comments:
Post a Comment