Monday, July 7, 2014

GUARDIOLA ANA MCHANGO KATIKA KIKOSI CHA UJERUMANI - MATTHAUS.

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Lothar Matthaus anaamini kuwa Pep Guardiola ana mchango wake katika kikosi cha nchi hiyo kwasababu kuna wachezaji wengi kutoka klabu ya Bayern Munich. Guardiola ambaye ni kocha wa zamani wa Barcelona alichukua mikoba ya kuinoa Bayern katika majira ya kiangazi mwaka jana na kuisaidia timu hiyo kushinda taji la Bundesliga katika msimu wake wa kwanza. Akihojiwa Matthaus alikiri kuwa ni kweli Guardiola ana mchango wake katika timu ya Ujerumani kutokana na wachezaji wengi wa Bayern waliopo ambapo wameleta aina yao ya kipekee katika uchezaji. Matthaus aliendelea kudai kuwa Guardiola ameshinda mataji mengi akiwa na Barcelona na amechukua baadhi ya mbinu alizokuwa akitumia huko na kuzileta Bayern na kutokana na Ujerumani na wachezaji wengi kutoka kwa mabingwa hao wa Bundesliga ndio maana anasema kocha huyo ana mkono wake katika timu hiyo. Kocha wa Ujerumani Joachim Loew anakabiliwa na kibarua kizito katika kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya fainali ya michuano wakati watakapochuana na wenyeji Brazil huko Belo Horozonte kesho.

No comments:

Post a Comment