Friday, July 11, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: ARGENTINA YANYUKWA FAINI NA FIFA KWA KOSA LA WACHEZAJI KUKACHA MIKUTANO NA WANAHABARI.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeitoza faini ya dola 336,000 Argentina kwa kushindwa kupeleka wachezaji katika mikutano minne ya wanahabari kabla ya mechi wakati wa michuano ya Kombe la Dunia. Kamati ya nidhamu ya FIFA imedai kuwa Argentina wamekiuka taratibu za vyombo vya habari na masoko katika mikutano ya kabla ya mechi kwenye michezo dhidi ya Nigeria, Uswis, Ubelgiji na Uholanzi ambayo kocha pekee ndio aliyekuwepo mkutanoni. Katika mikutano yote hiyo kocha anapaswa kuwepo na mchezaji awe wa kawaida au nahodha. Argentina watavaana na Ujerumani katika fainali ya michuano hiyo Jumapili, hawajatoa kauli yoyote ya kama wanakubali au kukata rufani kutokana na adhabu hiyo waliyopewa.

No comments:

Post a Comment