WINGA mahiri wa timu ya taifa ya Uholanzi, Arjen Robben amesema Argentina hawkaustahili kufika fainali ya michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuwafunga kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-2 jana usiku. Katika mchezo huo kumekuwa na nafasi chache za kufunga kwa timu zote hatua ambayo ilipelekea kumaliza bila ya kufungana baada ya muda wa nyongeza. Lakini safari hii bahati haikuwa kwa Uholanzi kama ilivyokuwa katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Costa Rica, kwani ni Argentina ndio walioonekana kutulia zaidi katika upigaji huku golikipa wao akiibuka shujaa kwa kuokoa matuta mawili. Akihojiwa Robben amesema Argentina hawkaustahili ushindi huo kwani hawakutengeneza nafasi nyingi za kufunga kama ilivyokuwa hivyo anaipa nafasi Ujerumani kunyakuwa taji hilo kwasababu ana marafiki wengi huko.

No comments:
Post a Comment