Tuesday, July 15, 2014

MABINGWA WA DUNIA UJERUMANI WAPOKEWA KISHUJAA NYUMBANI.

TIMU ya taifa ya soka ya Ujerumani imewasili nchini humo kwa kishindo wakiwa na kombe lao la ushindi walilolinyakua katika michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini Brazil Juzi. Maelfu ya mashabiki wa soka wamekuwa wakisubiri tangu asubuhi na mapema mjini Berlin kuwakaribisha mashujaa wao hao. 
Sherehe rasmi zitafanyika katika eneo la Brandenburg Gate, ambako wachezaji wataonyeshea kombe lao, ambalo walilishinda katika fainali ya michuano hiyo dhidi ya Argentina. Shangwe na vigelegele vimeshuhudiwa huku umati mkubwa wa watu ukitarajiwa kushuhudia kombe hilo ambalo litapitishwa katika miji yote. 
Mashabiki wengi wa soka nchini humo wamenunua jezi mpya za timu hiyo zenye alama ya nyota nne pembeni ya kifua kuashiria taji la nne kwa nchi hiyo katika Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment