Thursday, July 17, 2014

MADRID NDIO KLABU TAJIRI ZAIDI DUNIANI.

KLABU ya Real Madrid ya Hispania ndio imeongoza orodha ya vilabu vya michezo vyenye thamani zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes la Marekani. Madrid ambao walishinda michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu uliopita, wamekadiriwa kuwa na utajiri unaofikia dola bilioni 3.44. Orodha hiyo ya mwaka iliyotolewa jana imetawaliwa na vilabu vya soka ambapo Barcelona wako katika nafasi ya pili thamani yao ikiwa kiasi cha dola bilioni 3.2 na nafasi ya tatu inashikiliwa na Manchester United wakiwa na thamani ya dola bilioni 2.81. Forbes huwa wanapiga mahesabu yao ya thamani kwa kuzingatia usawa, madeni na mikataba ya uwanjani. Klabu nyingine katika orodha hiyo ni New York Yankees ya mchezo wa baseball kutoka Marekani ambayo ina thamani ya dola bilioni 2.5 na nafasi ya tano inashikiliwa na timu Mpira wa Kimarekani-NFL ya Dallas Cowboys ambayo ina thamani ya dola bilioni 2.3.

No comments:

Post a Comment