Wednesday, July 16, 2014

RENARD ATUMA MAOMBI YA KIBARUA IVORY COAST.

KOCHA Mfaransa Herve Renard ametuma maombi yake kwa ajili ya kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Ivory Coast na anaonekana kupewa nafasi kubwa ya kupata kazi hiyo. Renard mwenye umri wa miaka 45 ambaye zamani alikuwa akicheza nafasi ya beki amekuwa hana kibarua toka aliachia ngazi kuifundisha timu ya Sochaux msimu uliopita. Kocha huyo anaonekana kuwa vigezo vinavyohitajika kwa ajili ya kibarua hicho ambavyo mojawapo ni uwezo wa kuzungumza lugha ya kifaransa, uzoefu wa kufundhisha klabu au timu ya taifa na uzoefu wa soka la Afrika. Renard wakati akiifundisha Zambia alifanikiwa kushinda taji la Mataifa ya Afrika mwaka 2012 katika mchezo dhidi ya Ivory Coast ulioamuliwa kwa matuta huko jijini Libreville, Gabon. Kocha Sabri Lamouchi aliacha kibarua cha kuinoa Ivory Coast baada ya kushindwa kuivusha katika hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini Brazil mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment