NGULI wa soka wa zamani wa soka wa Brazil ambaye hivi sasa amehamia katika ulingo wa siasa, Romario amelikosoa Shirikisho la Soka la nchi hiyo-CBF na kulitaka kutafuta viongozi wapya. Wakati wa michuano ya Kombe la Dunia ilishuhudia mabingwa hao mara tano wa michuano hiyo wakitolewa katika hatua ya nusu fainali na waliokuja kuwa mabingwa Ujerumani ambapo Romario anafikiri viongozi waliokuwepo wanaendekeza rushwa ndio maana wameshindwa kufanya vyema. CBF ambayo ilifanya uchaguzi wake mwaka jana na kumteua Marco Polo del Nero wanatarajia kumkabidhi ofisi rasmi mwakani kutoka kwa Jose Maria Marin ili aongoze shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne inayokuja. Romario ambaye kwasasa ni mbunge amesema kwasasa CBF inahitaji safu mpya kabisa ya uongozi ili iweze kusahihisha makosa na tuhuma nyingi za rushwa zilizoliandama shirikisho hilo. Nguli huyo aliendelea kudai kuwa CBF haipaswi kuendeshwa na genge la watu fulani ambao tayari wameshaonyesha kushindwa shughuli hiyo, ila inatakiwa watu wanaoweza kuleta changamoto moto mpya ili wasiweze kupata tena aibu waliyopata katika michuano ya mwaka huu.

No comments:
Post a Comment