VYOMBO vya habari nchini Ufaransa vimeripoti kuwa wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa nchi hiyo, Karim Benzema amewadhalilisha waandishi wa habari wawili katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil. Taarifa iyo imedai kuwa tukio la kwanza lilitokea Juni 17 wakati Karim Djazir alipomsukumiza kwa kidole mwandishi. Djaziri alirudia tena tukio hilo Julai 5 saa chache baada ya Ufaransa kutolewa katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo na Ujerumani ambapo alimtolea maneno ya kuudhi na kumtishia mwandishi mwingine. Wakala huyo amekataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na tuhuma hizo zilizotolewa wakati alipoulizwa. Benzema mwenye umri wa miaka 26 ambaye anaichezea klabu ya Real Madrid, alifunga mabao matatu katika michuano hiyo ambayo yaliisaidia Ufaransa kuibuka vinara katika kundi lao kwenye michuano hiyo.

No comments:
Post a Comment