Wednesday, August 20, 2014

WENGER ACHUKIZWA NA MWAMUZI BAADA YA ARSENAL KUTOA SARE NA BESIKTAS.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amechukizwa na uamuzi wa kutolewa nje kwa Aaron Ramsey wakati kikosi chake kilipong’ang’aniwa sare ya bila kufungana na Besiktas katika mchezo wa mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jana usiku. Kadi zote mbili za njano alizopewa Ramsey zimetokana na kuwavuta wachezaji wa Besiktas, na kadi nyekundu aliyopewa inamaanisha kuwa takosa mchezo wa mkondo wa pili utakaofanyika katika Uwanja wa Emirates Agosti 27 mwaka huu. Akihojiwa Wenger amesema kadi zote mbili za njano alizopewa Ramsey hakustahili hivyo anadhani mwamuzi hakuwa sahihi haswa kutokana na faulo zingine zilizochezwa. Matumaini ya Arsenal kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa msimu wa 17 mfululizo sasa imekuwa mashakani baada ya mchezo huo wa kwanza uliochezwa jijini Instabul kumalizika kwa sare.

No comments:

Post a Comment