KLABU ya Tottenham Hotspurs limepeleka malalamiko yao Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kufuatia kuonyeshwa kwa mabango yenye kulenga ubaguzi na mashabiki wa Partizan Belgrade. Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino ameelezea bango hilo kama jambo lisilokuwa na heshima na lisilokubalika. Spurs walishindwa kutamba ugenini kwa kung’ang’aniwa sare na wenyeji ya bila kufungana katika Uwanja wa Partizani. Maofisa wa Spurs waliwataarifu UEFA juu ya uwepo wa bango hilo kabla ya mapumziko na wajumbe wake walilipiga picha kama ushahidi baada ya mchezo huo. Mwaka 2007, Partizan walitolewa katika michuano ya Kombe la UEFA na kutozwa faini kwa vurugu wakati wa mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano hiyo dhidi ya Zrinjski Mostar.
No comments:
Post a Comment