Wednesday, October 22, 2014

BALOTELLI AZUA JAMBO TENA LIVERPOOL IKICHAPWA 3-0 NA REAL MADRID.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Mario Balotelli anakabiliwa na karipio kutoka kwa meneja wake Brandan Rodgers baada ya kubadilishana fulana na beki wa Real Madrid Pepe katika muda wa mapumziko wakati timu hiyo ilipotandikwa kwa mabao 3-0 katika Uwanja wa Anfield. Balotelli alifanya tukio hilo wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao matatu katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo baadae mshambuliaji huyo alitolewa. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Rodgers amesema jambo hakulifurahia kwani kama mchezaji anataka kubadiishana fulana na mwenzake anapswa kusubiri mpaka mchezo utakapomalizika. Rodgers ambaye pia amewahi kumvaa beki wake Mamadou Sakho ambaye alifanya tukio hilo kama hilo na Samuel Eto’o wakati akiwa Chelsea msimu uliopita amesema suala hilo ni ndani na atakabiliana nalo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kubadilishana fulana wakati wa mapumziko na jambo ambalo halifanyikagi katika timu hiyo hivyo inapaswa wachezaji wake wakaelewa hilo.

No comments:

Post a Comment