Wednesday, October 8, 2014

DONOVAN KUCHEZA MECHI YAKE YA MWISHO YA KUAGA MAREKANI.

MCHEZAJI mkongwe London Donovan anatarajiwa kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Marekani katika mechi yake ya mwisho Ijumaa hii. Kocha wa Marekani Jurgen Klinsmann amesema jana kuwa mshambuliaji huyo wa klabu ya Los Angeles Galaxy mwenye umri wa miaka 32 ataanza na kucheza dakika takribani 30 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ecuador utakaochezwa huko East Hartford, Connecticut. Donovan ambaye anatarajia kustaafu rasmi soka mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu ya Soka ya Marekani, ameifungia nchi hiyo mabao 57. Mchezo huo utakuwa ni wa 157 kwa Donovan ambaye amecheza fainali tatu za Kombe la Dunia lakini aliachwa katika michuano ya mwaka huu iliyofanyika nchini Brazil kutokana na kushindwa kuelewana na Klinsmann.

No comments:

Post a Comment