NGULI wa soka wa Uholanzi, Ronald de Boer amedai kuwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Guus Hiddink ameishiwa baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 2-0 na Iceland katika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016. Mabao mawili yaliyofungwa na Gylfi Sigurdsson yalitosha kuwapata ushindi wa kushtusha Iceland dhidi ya Uholanzi ambao ni walikuwa washindi wa tatu katika Kombe la Dunia nchini Brazil ambao sasa wanakuwa wamepoteza michezo mitatu kati ya minne waliyocheza chini Hiddink mwenye umri wa miaka 67. De Boer ambaye amewahi kuiwakilisha nchi hiyo katika fainali mbili za Kombe la Dunia na mbili za michuano ya Ulaya anadhani Ronald Koeman alistahili kuchukua nafasi ya Louis van Gaal baada ya Kombe la Dunia. Akihojiwa De Boer amesema katika macho yake haoni kama Hiddink ana mipango ya madhubuti ya kuiwezesha timu hiyo kushinda. De Boer aliendelea kudai kuwa kuna michezo mingi ya kucheza na kubadilika lakini shinikizo limekuwa kubwa sana kwa Hiddink hivi sasa kwasababu uteuzi wake ulikosololewa na watu wengi.

No comments:
Post a Comment