MENEJA wa klabu ya Benfica, Jorge Jesus amesisitiza kuwa alipaswa kujumuishwa katika orodha ya makocha 10 watakaogombea tuzo ya kocha bora wa mwaka, akidai kuwa baada ya walioukuwemo katika orodha hiyo wamepata mafanikio madogo kuliko yeye. Akihojiwa Jesus ambaye aliiongoza Benfica kushinda mataji matatu ya nyumbani msimu uliopita huku akifika fainali ya michuano ya Europa League amesema hajui ni vigezo vipi vilivyotumika kuteua orodha hiyo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kuna baadhi ya makocha walioteuliwa wamepata mafanikio kiduchu kuliko yeye la anashangaa wamejumuishwa kwenye orodha hiyo. Jesus amesema kutokana na jinsi orodha hiyo ilivyo anadhani hata yeye alipaswa kuwemo kutokana na mafanikio aliyopata akiwa na Benfica msimu uliopita. Orodha hiyo makocha walioteuliwa na timu zao katika ni pamoja na Carlo Ancelotti (Real Madrid), Antonio Conte (Italy/Juventus), Pep Guardiola (Bayern Munich), Juergen Klinsmann (United States), Joachim Loew (Germany). Wengine ni Jose Mourinho (Chelsea), Manuel Pellegrini (Manchester City), Alejandro Sabella (Argentina), Diego Simeone (Atletico Madrid) andLouis van Gaal (Netherlands) were on the Fifa shortlist announced on Wednesday.
No comments:
Post a Comment