CHAMA cha Wachezaji Soka wa Kulipwa-PFA kimeponda mpango wa Ligi ya Soka nchini Uingereza kutumia viwanja vyenye nyasi bandia katika ligi daraja la kwanza na pili. Ofisa mkuu msaidizi wa PFA, Simon Barker amesema wameshangazwa na kusikitizshwa na uamuzi uliotolewa hivi karibuni. Barker aliendelea kudai kuwa wakiwa kama wawakilishi wa wachezaji walipaswa kushirikishwa katika maamuzi hayo kabla ya wenyeviti wa vilabu hawajatoa uamuzi kwani wanaocheza katika viwanja ni wajumbe wao. Kiongozi huyo wa PFA aliongeza kuwa Chama cha Mameneja wa Ligi pia hakikushirikishwa na kuongeza wasiwasi juu ya majeruhi na athari zitakazotokea wakati wakitumia viwanja hivyo. Mapema Septemba mwaka huu wenyeviti 26 kati ya 46 wa vilabu walikubalia mpango huo mpya wa viwanja vya nyasi za bandia mapendekezo ambayo yanatarajiwa kupitishwa katika mkutano mwingine Novemba.

No comments:
Post a Comment