Tuesday, November 4, 2014

AL HILAL YALALAMIKIA MWAMUZI BAADA YA KUSHINDWA KUNYAKUWA TAJI LA LIGI YA MABINGWA LA ASIA.

KLABU ya Al-Hilal ya Saudi Arabia imetaka uchunguzi rasmi kufanyika kuhusiana na uteuzi wa mwamuzi aliyechezesha fainali ya michuano ya Klabu Bingwa barani Asia, ambapo walifungwa kwa jumla ya bao 1-0 na klabu ya Sydney Wanderers mwishoni mwa wiki iliyopita. Al-Hilal walishindwa kufuta matokeo ya sare ya bila ya kufungana katika mchezo wa fainali ya mkondo wa pili iliyochezwa jijini Riyadh, ambapo walishuhudia mwamuzi Yuichi Nishimura kutoka Japan akiwakatalia penati tatu. Katika taarifa ya klabu hiyo, imedai kuwa hatua za makusudi zinapaswa kuchukuliwa kukabiliana na masuala hayo ili mchezo wa soka uweze kuwa na usawa. Hii ni mara ya pili kwa Nishimura kuingia katika mgogoro katika mechi alizochezesha baada ya kuwapa wenyeji Brazil penati yenye utata katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia dhidi ya Croatia. Klabu hiyo pia inalalamikia uwezo wa mwamuzi kutoka Iran Alireza Faghani aliyechezesha fainali ya mkondo wa kwanza ambapo Al-Hilal walichapwa bao 1-0 pamoja kumiliki mchezo muda wote.

No comments:

Post a Comment