Tuesday, November 11, 2014

KITENDAWILI CHA AFCON BADO KUTEGULIWA.

MAANDALIZI kwa ajili ya mechi za kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon mwakani yanaendelea kama kawaida wiki hii pamoja na ukweli kwamba michuano hioyo inaweza isifanyike na kufanya mechi hizo mbili za mwisho kuwa hazina maana yeyote. Timu zinatarajiwa kucheza mechi zao hizo muhimu Ijumaa na Jumamosi hii kabla ya kumalizia mechi za mwisho wiki ijayo ambapo timu 15 zitafuzu kutokana na msimamo wa makundi yao. Algeria na Cape Verde wao tayari wamejihakikishia nafasi ya kushiriki michuano hiyo. Jumla ya timu 28 zinagombania nafasi ya kushiriki michuano hiyo Januari mwakani ambap kuna uwezekano mkubwa wa Morocco kunyang'anywa haki ya kuwwa mwenyeji na michuano hiyo kuhamishwa sehemu nyingine au kusitishwa kabisa. Morocco walikuwa wakitaka michuano hiyo kusogezwa mbele kwasababu ya hofui bya kusambaa kwa ubonjwa wa Ebola lakini Shirikisho la Soka la Afrika limepinga ombi hilo na kudai michuano hiyo itafanyika kama ilivypangwa. Kikao cha kamati ya utendaji ya CAf kinachokutana leo jijini Cairo ndicho kitakachoamua wapi na lini fainali hizo zitafanyika.

No comments:

Post a Comment