MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Algeria na klabu ya FC Porto, Yacine Brahimi ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika inayotolewa na Shirika la Utangazaji la BBC. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Algeria kushinda tuzo hiyo ambayo hupigiwa kura na mashabiki kutoka pande mbalimbali za bara la Afrika. Akihojiwa Brahimi amesema ni heshima kubwa kwake kushinda tuzo hiyo muhimu na anawashukuru watu wote nchini kwake na popote pale ambao walimpigia kura. Brahimi alikuwa akichuana na Yaya Toure na Gervinho kutoka Ivory Coast, Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Gabon na Vincent Enyeama kutoka Nigeria.

No comments:
Post a Comment