Sunday, December 14, 2014

RONALDO ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA KUTOKA NJE YA UINGEREZA.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kushinda tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka huu inayoandaliwa na BBC kwa wachezaji wasio raia wa Uingereza. Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 alishinda tuzo ya mchezaji wa mwaka miezi 11 iliyopita. Nyota huyo ambaye amefunga mabao 281 katika mechi 267 alizoichezea Madrid, aliwashukuru BBC kwa kumchagua pamoja na mashabiki wake wa zamani wa Uingereza. Ronaldo alishinda tuzo akiwazidi mchezaji tenisi mahiri wa Marekani Serena Williams, Bondia Floyd Mayweather na dereva wa MotoGP Marc Marquez. Nyota huyo anakuwa mchezaji soka wa pili kushinda tuzo hiyo kwa karne hii baada ya nguli wa Brazil Ronaldo Di Lima kushinda tuzo hiyo mwaka 2002.

No comments:

Post a Comment