KLABU ya Barcelona imemtimua golikipa wa zamani Andoni Zubizarreta katika nafasi yake ya ukurugenzi wa michezo wa timu hiyo. Zubizarreta mwenye umri wa miaka 53, alipewa wadhifa huo katika majira ya kiangazi mwaka 2010 baada ya kuondoka kwa Txiki Begiristian ambaye sasa ndiye mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Manchester City. Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amethibitisha kutengua mkataba wa Zubizarreta huku akimshukuru kwa kazi yake kubwa aliyofanya katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Muda mchache baada ya kutangazwa kutimuliwa kwa Zubizarreta, naye nahodha wa zamani wa klabu hiyo Carlos Puyol alitangaza kujiuzulu nafasi ya kama mkurugenzi wa msaizidi wa michezo. Puyol aliandika katika ukurasa wake facebook kuwa katika kipindi cha miezi mitatu na nusu aliyoshikilia wadhifa huo amejifunza mambo mengi ambayo yatamfanya kuimarika zaidi ili baadae aweze kurejea tena.

No comments:
Post a Comment