Monday, January 5, 2015

JUVENTUS KUKAMULIWA EURO MILIONI 20 KWA AJILI YA SNEIJDER.

WAKALA wa kiungo wa klabu ya Galatasaray, Wesley Sneijder amedai kuwa klabu ya Juventus italazimika kutoa kitita cha euro milioni 20 kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo. Sneijder mwenye umri wa miaka 30 alihamia Galatasaray katikati ya msimu wa 2012-2013 baada ya kuondoka Inter Milan. Lakini katika wiki za karibuni nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekuwa akihusishwa na kuondoka katika klabu hiyo ya Uturuki huku Juventus wakitajwa kutaka huduma ya mchezaji huyo. Hata hivyo wakala wa Sneijder, Guido Albers amesisitiza kuwa mteja wake hana mpango wa kuondoka Instabul ila kama Juventus walilazimisha uhamisho huo watalazimika kutoa kitita cha euro milioni 20 ili kutengua mkataba wake.

No comments:

Post a Comment