Saturday, January 3, 2015

PODOLSKI ATIMKIA INTER MILAN.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Arsenal, Lukas Podolski amezungumzia furaha yake ya kukaribia kukamilisha mkopo wake kwenda klabu ya Inter Milan. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alitupilia mbali ofa ya kwanza ya Inter akiwataka waimarishe zaidi na sasa inaoenekana timu hizo kufikia makubaliano kwa nyota huyo kwenda Italia kwa msimu mzima uliobakia. Podolski alitua jijini Milan jana usiku na kupokewa na mashabiki kadhaa wa Inter huku akitarajiw akufanyiwa vipimo vya afya leo. Akihojiwa na wanahabari Podolski amesema anafurahia kujiunga na Inter na anategemea mengi mazuri katika safari yake hiyo mpya kwakuwa anaifahamu ligi ya Italia vizuri.

No comments:

Post a Comment