KLABU ya Zamalek ya Misri imeanza kufanya mazungumzo na kocha Mreno Jorvan Vieira ili aweze kuinoa timu hiyo kwa msimu uliobakia. Aliyekuwa kocha wa timu hiyo Jamie Pacheco aliondoka wiki iliyopita kufuatia kutoelewana na mwenyekiti wa timu hiyo Mortada Mansour. Kocha msaidizi Mohamed Salah ndiye amepewa majukumu ya kuisimamia timu hiyo mpaka hapo atakapopatikana kocha mpya. Vieira mwenye umri wa miaka 61 aliingoza Zamalek katika msimu wa 2012-2013 kabla ya kuondoka baada ya kugoma kuongeza mkataba wake. Zamalek kwasasa ndio wanaoongoza Ligi Kuu nchini humo wakiwa wamefikisha alama 40.

No comments:
Post a Comment