OFISA mkuu wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke amedai kuwa Mario Gotze na Robert Lewandowski sio wachezaji pekee wa timu hiyo ambao Bayern Munich walikuwa wamepania kuwasajili. Dortmund waliizidi maarifa Bayern na kunyakuwa taji la Bundesliga msimu wa 2010-2011 na 2011-2012, wakati pia wakiichapa Bayern kwa mabao 5-2 katika fainali ya DFB Pokal msimu huohuo. Hata hivyo pamoja na kuwapoteza Gotze na Lewandowski pekee waliokwenda kwa mahasimu wao hao bado Dortmund imekuwa ikisuasua katika ligi. Akihojiwa Watzke amesema Bayern waliwachukua wachezaji wao wawili muhimu na kuendelea kuwa mahasimu wao hao abado walikuwa wakihitaji wachezaji zaidi. Watzke aliendelea kudai kuwa Bayern waliamua kuwavuruga kwani walikuwa tishio kwao kutokana na mafanikio waliyopata mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment