Wednesday, March 4, 2015

TETESI ZA USAJILI ULAYA: LIVERPOOL, MADRID ZAWINDA KINDA LA VILLARREAL, MAN UNITED YAMTENGEA DANILO PAUNDI MILIONI 37.

KATIKA habari za tetesi za usajili zilizopamba vichwa vya habari vya magazeti na mitandao barani Ulaya ni pamoja na klabu za Liverpool na Real Madrid zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Villarreal Luciano Vietto mwenye umri wa miaka 21. Kwa mujibu wa wakala wa mchezo huyo klabu hizo zitalazimika kutoka kitita cha paundi milioni saba kama watahitaji saini yake. Klabu ya Queens Park Rangers-QPR imeanza mazungumzo ya mkataba mpya na beki chipukizi Darnell Furlong mwenye umri wa miaka 19 baada ya vilabu kadhaa kuonyesha nia ya kumtaka. Golikipa wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech, Petr Cech mwenye umri wa miaka 32 anaweza kuondoka Chelsea mwishoni mwa msimu baada ya kupoteza nafasi yake kama golikipa namba moja wa klabu hiyo. Manchester United imeanza mazungumzo ya kutaka kumsajili beki wa kulia wa FC Porto Danilo mwenye umri wa miaka 23 na wako tayari kutoa kitita cha paundi milioni 37 kwa ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa Brazil. Meneja wa klabu ya Everton Roberto Martinez amezungumza na klabu ya Barcelona juu ya uwezekano wa kumsajili kiungo wao Sergi Roberto mwenye umri wa miaka 23. Klabu ya Arsenal inasubiri jibu baada ya kutuma ofa kwa mshambuliaji wa Boca Junior Jonathan Calleri mwenye umri wa miaka 21.

No comments:

Post a Comment