MENEJA wa Liverpool, Brendan Rodgers amebainisha kuwa tayari ameshazungumza na Steven Gerrard kuhusu uwezekano wa kurejea katika klabu hiyo siku za usoni. Gerrard anatarajiwa kucheza mechi yake ya mwisho katika Uwanja wa Anfield akiwa na Liverpool kesho kabla ya kuhamia katika klabu ya Los Angeles Galaxy ya Marekani mwishoni mwa msimu. Nahodha huyo wa Liverpool ambaye ameichezea klabu hiyo kea kipindi cha miaka 17 tayari ameonyesha nia ya kurejea akiwa kocha na Rodgers anadhani kuna uwezekano mkubwa wa hilo. Akihojiwa Rodgers amesema Gerrard hajaondoka moja kwa moja kwani in mtu ambaye angependa kufanya naye kazi pindi atakapotundika daruga zake.
No comments:
Post a Comment