Tuesday, June 23, 2015

BEKI MKONGWE WA PARAGUAY AWAONYA WENZAKE KUHUSU BRAZIL.

BEKI wa timu ya taifa ya Paraguay, Paulo da Silva amewataka wachezaji wenzake kuwa makini katika mchezo wao war obo fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya Brazil, akisisitiza wapinzani wao hao bado in hatari pamoja na kumkosa nahodha wao Neymar. Paraguay watakwaana na Brazil Jumamosi hii huku wakimkosa neymar ambaye amelimwa adhabu ya kutocheza mechi nne kufuatia kipigo cha bao 1-0 walichopata kutoka kwa Colombia Alhamisi iliyopita. Lakini Da Silva ambaye alikuwepo katika kikosi cha Paraguay ambacho kiliing’oa Brazil kwa changamoto ya mikwaju ya penati mwaka 2011 katika michuano hiyo, bado anadhani in hatari pamoja na kumkosa nyota wake huyo. Mkongwe huyo amesema Neymar in mchezaji muhimu kea Brazil lakini pamoja na kutokuwepo timu hiyo bado inaweza kuwa na madhara kwao kwani wapo nyota wengine wanaoweza kutoa matokeo yanayohitajika. Da Silva aliendelea kudai jambo la msingi in kutobweteka na kuwa tayari kwa lolote kwenye mchezo huo kama wanataka kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment