MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne amethibitisha kuwa Manchester City wamefanya mawasiliano na wakala wake lakini amesisitiza klabu yeyote itakayomuhitaji lazima ikubaliane na Wolfsburg kama wanataka kumsajili majira haya ya kiangazi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, ameimarika na kuwa mmoja kati ya wachezaji nyota chipukizi baada ya kumaliza msimu akiwa amefunga mabao 15 na kusaidia mengine 25 akiwa na Wolfsburg. Klabu za Bayern Munich na Paris Saint-Germain pia zimeonyesha nia ya kumsajili De Bruyne ambaye inaaminika Wolfsburg watataka kumuuza kwa euro milioni 49 ikiwa in mara mbili ya kiwango alichonunuliwa akitokea Chelsea Januari mwaka jana. Akihojiwa De Bruyne amesema anajua kuwa kuna mazungumzo yamefanyika kati ya wakala wake na City lakini kama anavyowaambia wote kama mtu anataka chochote anapswa kwenda kuzungumza na Wolfsburg kwanza na sio yeye.
No comments:
Post a Comment