KIUNGO mahiri Jordan Henderson ana uhakika wa kuvaa viatu vua Steven Gerrard kama nahodh mpya wa Liverpool na yuko tayari kuongoza safu ya kiungo ya timu hiyo msimu ujao. Henderson ambaye amesaini mkataba mpya hivi karibuni anapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwa nahodha mpya na meneja wa timu hiyo Brendan Rodgers kufuatia kuondoka kea Gerrard kwenda klabu ya Los Angeles Galaxy ya Marekani. Akihojiwa Henderson amesema siku zote amekuwa akitaka kupewa majukumu zaidi kipindi hiki kea anajiona kama ameshakuwa na umri wa kutosha. Nyota huyo amesema wakati akiwa nahodha msaidizi amekuwa akitajaribu kujituma kadri ya uwezo wake na kujivunza kadri anavyoweza kutoka kea Gerrard.
No comments:
Post a Comment