Wednesday, June 10, 2015

KHEDIRA AKIRI KUPATA WAKATI MGUMU KUONDOKA MADRID.

KIUNGO mpya wa Juventus, Sami Khedira amekiri uamuzi wa kuondoka Real Madrid ulikuwa mgumu lakini ana uhakika wa kushinda mataji zaidi akiwa jijini Turin. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Madrid mwaka 2010 na alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha timu hiyo chini Jose Mourinho lakini alishindwa kabisa kupata namba chini ya Carlo Ancelotti baada ya kupona majeraha mabaya aliyopata mwaka 2013. Matokeo hayo ndio yaliyofanya klabu kutomuongeza mkataba mwingine na kumfanya kujiunga na Juventus kama mchezaji huru. Akihojiwa Khedira amesema haukuwa uamuzi rahisi kwasababu alikuwa akiipenda Madrid lakini hakuna marefu yasiyokuwa na ncha kwani sasa anataka kuanza maisha mapya na kuisaidia Juventus kuendelea kung’aa Ulaya. Huo unakuwa usajili wa pili kea Juventus ambao tayari walikuwa wameshamnasa Paulo Dybala kea kitita cha euro milioni 40 kutoka AS Roma.

No comments:

Post a Comment