Wednesday, June 10, 2015

LEBRON JAMES AENDELEA KUING'ARISHA CAVALIERS.

MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu LeBron James ameendelea kuing’arisha timu yake ya Cleveland Cavaliers baada ya kufunga vikapu 40 vilivyosaidia kuifunga Golden State Warriors kwa jumla ya vikapu 96-91 katika fainali ya tatu kati ya saba za NBA. Nyota huyo wa zamani wa timu ya Miami Heat pia alidaka rebound 12 na kutoa nafasi nane za kufunga hivyo kuifanya Cavaliers sasa kuongoza kwa mechi 2-1. James mwenye umri wa miaka 30 anacheza fainali yake ya tano mfululizo ya NBA na tayari ameshafunga jumla ya vikapu 123 katika michezo hiyo mitatu aliyocheza. Timu hizo zinatarajiwa kucheza mechi nyingine moja katika Uwanja wa Quickens Loan Arena kesho kabla ya kurejea tena Oakland Jumapili hii kea ajili ya mechi ya tano.

No comments:

Post a Comment