Friday, June 12, 2015

LIVERPOOL YAKATAA PAUNDI MILIONI 25 ZA MAN CITY KWA AJILI YA STERLING.

KLABU ya Liverpool imekataa ofa ya paundi milioni 25 zilizotolewa na Manchester City kwa ajili ya mshambuliaji Raheem Sterling. Liverpool wanamthaminisha nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye pia anahusisha na tetesi za kutakiwa Arsenal na Real Madrid, kufikia paundi milioni 50. Sterling mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Liverpool akitokea Queens Park Rangers mwaka 2010 na yuko chini ya mkataba mpaka mwaka 2017. Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers alisema mwezi uliopita kuwa anamtegemea nyota huyo kubakia Anfield mpaka mkataba wake utakapokwisha baada ua kukataa kusaini mkataba mpya ambao ungemuwezesha kulipwa kitita cha paundi 100,000 kwa wiki.

No comments:

Post a Comment