TIMU ya taifa ya Mali imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kea vijana chini ya umri wa miaka 20 inayoendelea huko New Zealand baada ya kuitandika Ghana mabao 3-0. Ghana ambao walikuwa mabingwa wa michuano hiyo mwaka 2009, waliingia katika mchezo huo wakipewa nafasi kubwa baada ya kuitandika Argentina na kuvuka katika kundi B wakiwa vinara. Lakini mambo yalikuwa tofauti walipoingia uwanjani kwani Mali walionesha kiwango cha hali ya juu ambapo juhudi zao hizo zilizaa matunda na kuwafanya kuibuka kiidedea katika mchezo huo. Mali sasa watakwaana na aidha Ujerumani au Nigeria katika hatua hiyo ya robo fainali.
No comments:
Post a Comment