MSHAMBULIAJI nyota wa Brazil, Neymar anaamini kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kina wachezaji wenye ubora na uzoefu unaohitaji kea ajili ya kunyakuwa taji la michuano ya Copa America inayoendelea nchini Chile bila uwepo wake. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 aliondoka katika kambi ya Brazil jana baada ya kulimwa adhabu ya kutocheza mechi nne kwa kosa la kumpiga kichwa Jeison Murillo wakati wa mchezo ambao Brazil ilitandikwa bao 1-0 na Colombia Alhamisi iliyopita. Lakini pamoja na kutokuwepo Neymar bado ana uhakika wachezaji wenzake waliobakia wana uwezo wa kuipeleka timu hiyo fainali na hatimaye kunyakuwa taji. Neymar mwenye umri wa miaka 23, amesema anadhani Brazil bado ina uhai bila uwepo wake kwani wachezaji wenzake wameonyesha kuwa wanaweza kushinda mechi na taji la michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment