RAIS wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amethibitisha Pepe Reina atafanyiwa vipimo vya afya leo ikiwa in sehemu ya kukamilisha uhamisho wake wa kurejea katika klabu hiyo. Reina alijiunga na Bayern Munich Agosti mwaka jana lakini amefnikiwa kucheza mechi tatu pekee kea mabingwa hao wa Bundesliga kutokana na kuwa chini ya golikipa namba moja Manuel Neuer. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania aliichezea Napoli mechi 43 katika msimu wa 2013-2014 ambapo alikuwa akicheza kwa mkopo kutoka klabu ya Liverpool. Akihojiwa Laurentiis amesema Reina atafanyiwa vipimo vya afya na kama kila kitakwenda sawa moja kea moja atasaini mkataba. Kwa upande mwingine rais huyo amekuwa akimuunga mkono meneja mpya Maurizio Sarri kuendeleza kazi nzuri iliyoachwa na Rafael Benitez msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment