Monday, June 8, 2015

PIRLO AKANUSHA KUONDOKA JUVENTUS.

KIUNGO mahiri wa Juventus, Andrea Pirlo amesisitiza kuwa machozi yaliyomtoka baada ya mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yalikuwa in kutokana na matokeo na sio kwamba alikuwa akiaga. Nyota huyo wa kimataifa wa Italia amewahi kukiri huko nyuma kuwa angependa kuondoka Turin kama Juventus wangeifunga Barcelona jijini Berlin pamoja na kuwa bado na mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Hata hivyo, wakati mkongwe huyo akimwaga chozi baada ya kutandikwa mabao 3-1 na Barcelona, wachambuzi wengi wa soka walioanisha tukio hilo na nia yake ya kutaka kuondoka. Akihojiwa Pirlo amesema sio kweli kwanza alilia kwasababu mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwake bali matokeo waliyopata ndio yaliyokuwa yakimhuzunisha.

No comments:

Post a Comment