Friday, July 10, 2015

MONK AMWAGA WINO MIAKA MITATU SWANSEA.

MENEJA wa Swansea City Garry Monk amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo yenye maskani yake Uwanja wa Liberty. Beki huyo wa zamani alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kutoka kwa Michael Laudrup Februari mwaka jana na kuiongoza kumaliza kumaliza katika nafasi za juu katika Ligi Kuu msimu uliopita. Mwenyekiti wa Swansea, Huw Jenkins alikaririwa na mtandao wa klabu akithibitisha taarifa hizo huku akidai mkataba huo umekuwa kama zawadi kwa Monk kutokana na kazi nzuri aliyofanya msimu uliopita. Jenkins aliendelea kudai kuwa kutokana na mipngo endelevu waliyonayo wanadhani Monk ndiye atakuwa meneja sahihi kuipeleka klabu hiyo mbele zaidi.

No comments:

Post a Comment